Bima ya chombo cha usafiri ni bidhaa ya bima ambayo inalenga kukulinda na hasara endapo chombo chako cha moto kitaharibika, au madai ya watu wengine yatapotolewa. Hasara inaweza kutokea kwa ajali (moto, mlipuko, kugonga, n.k.), wizi na matukio mengine mengi yanayoweza kulipwa baada ya madai kufanyika.
Huduma hii ya bima ni mahususi kwa aina mbalimbali za vyombo vya moto kama vile, Gari, Pikipiki, Bajaj, Basi, Lori, Tanker, trekta na mengine, yaliyosajiliwa kwa matumizi ya binafsi na kibiashara.
Wateja wa Tigo Pesa wanaweza kusajili magari yao, kununua bima ndogo, na kufungua madai ya fidia, kwa kutumia simu zao za mkononi, kupitia Tigo Pesa.
Kwa maelezo zaidi vigezo na masharti tembelea https://web.bimapap.co.tz/docs/policy.pdf